1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Vikwazo kuendelea kuwaathiri Wapalestina.

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHJ

Marekani imesema jana kuwa vikwazo vya kimataifa vya misaada vilivyowekwa dhidi ya serikali inayoongozwa na chama cha Hamas itaendelea kubaki.

Lakini , mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya , Javier Solana , amesema kuwa anamatumaini kuwa Wapalestina watafikia masharti hivi karibuni ya kuondoa vikwazo hivyo.

Marekani, umoja wa Ulaya , Russia na umoja wa mataifa zinadai kuwa Hamas waitambue Israel, wakane matumizi ya nguvu na kukubali makubaliano yaliyopo kabla ya vikwazo hivyo kuondolewa.

Hata hivyo , tawi la kijeshi la Hamas jana lilidai kuhusika na shambulio la risasi dhidi ya mfanyakazi mmoja wa Kiisrael karibu na ukingo wa magharibi na kurusha makombora mawili dhidi ya kituo cha kijeshi cha Israel.