1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Vikwazo vipya dhidi ya Iran

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cc

Marekani imeweka vikwazo vipya dhidi ya Iran ikiilaumu nchi hiyo kuwa inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia na inaunga mkono ugaidi katika nchi za ngámbo.Vikwazo vilivyotangazwa na Waziri wa Nje wa Marekani,Condoleezza Rice na Waziri wa Fedha,Henry Paulson mjini Washington vinalenga benki tatu za Iran,makampuni tisa yanayohusika na petroli,ujenzi na usafiri ambayo hudhibitiwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi-IRGC.