1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush asema Gonzales alipakwa matope kisiasa

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVD

Mwanasheria mkuu wa Marekani Alberto Gonzales alijiuzulu hapo jana baada ya kipindi kigumu cha kukosolewa na wapinzani wake kutoka vyama vya Republican na Demokratic.

Gonzales mshirika mkubwa wa rais Bush ametangaza kwamba atajiuzulu kuanzia tarehe 17 mwezi ujao.Kazi yake Gonzales imekuwa ikitiliwa shaka na wapinzani wake hasa baada ya kutokea kashfa ya kuwafuta kazi waongozaji mashtaka wanane wa serikali hatua ambayo ilitajwa na wengi kuwa iliyochochewa kisiasa.

Akizungumzia kujiuzulu kwa mwanasheria huyo rais Bush alisema,

‘’ inasikitisha kwamba katika wakati kama huu mtu mwenye kipaji na wakutegemewa kama Gonzales anazuiwa kufanya kazi muhimu kutokana na kupakwa matope jina lake kwa sababu za kisiasa.’’

Chama cha Demokratic kimeapa kuendelea kufanya uchunguzi kuona ikiwa Gonzales alishirikiana na ikulu katika kuwafurusha kazini waendesha mashtaka 8 waserikali kwa sababu za kisiasa.