1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Wauguzi wahukumiwa kifungo cha maisha sio kifo

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhc

Mataifa ya magharibi yamepokea vizuri uamuzi wa mahakama kuu nchini Libya kuhusiana na kesi iliyowakabili wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa Palestina walioshtakiwa kwa kuwaambukiza zaidi ya watoto 400 virusi vya Ukimwi.Wafanyikazi hao wa huduma za afya wamehukumiwa jela kifungo cha maisha badala ya kifo iliyotolewa awali.

Kiongozi wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso anatoa wito wa wauguzi na daktari kurejeshwa barani Ulaya.Marekani na nchi ya Bulgaria nazo pia zinaitikia mwito huo wa kurejeshwa nchini Bulgaria.

Wauguzi hao 5 na daktari mmoja wanakanusha kuwaambukiza watoto hao virusi vya ukimwi na kushikilia kuwa waliungama kwasababu ya mateso.Wataalam wa kigeni wanasema kuwa usafi duni katika hospitali ya Benghazi huenda ulichangia katika maambukizi hayo.

Manesi hao na daktari wanazuiliwa nchini Libya tangu mwaka ’99.

Bado haijulikani iwapo watarejeshwa nchini Bulgaria.Nchi ya Bulgaria ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwanzoni mwa mwaka huu.