1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watetea usahi wa hali ya ehwa watunukiwa zawadi ya amani ya Nobel

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GO

Oslo:

Tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2007,wametunukiwa kwa pamoja,makamo wa rais wa zamani wa Marekani al Gore na tume ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya hali ya hewa.Kamati kuu ya Nobel imesifu juhudi za wateule hao katika kukusanya maelezo na kuwatanabahisha walimwengu juu ya hatari inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Juhudi zao katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na hatua zinazofaa kuchukuliwa katika kupambana na mabadiliko hayo ni miongoni mwa sababu za kutunukiwa zawadi ya amani ya Nobel,amesema hayo mwenyekiti wa kamati ya Nobel,Ole Danbolt Mjoes.Al Gore na wawakilishi wa tume ya Umoja wa mataifa inayosimamia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa,watatunukiwa tuzo hiyo yenye thamani ya yuro miliono moja na laki moja december 10 ijayo,siku ya kufariki dunia muasisi wa tuzo hii,Alfred Nobel.