1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wathailand wamuaga mfalme wao mpendwa Bhumibol

Iddi Ssessanga
26 Oktoba 2017

Mamia kwa maelfu ya Wathailand walikusanyika mjini Bangkok kwa ajili ya kumuaga mfalme wao Bhumibol Adulyadej, ambaye alifariki mwaka jana baada ya kukalia kiti cha ufalme kwa miongo saba.

https://p.dw.com/p/2mWLI
Thailand Einäscherungszeremonie von König Bhumibol
Picha: Getty Images/AFP/R. Schmidt

Kufikia alfajiri takribani watu 200,000 walikuwa wamekusanyika karibu na kasri la mfalme kumuaga mfalme wao anaejulikana kama "baba wa taifa," kabla ya tukio la kuchoma mabaki ya mwili wake lililokuwa limepangwa kufanyika baadaye Alhamisi.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa wamebeba picha za mfalme huyo. Kimbwi lenye urefu wa mita 49 pamoja na banda la msiba huo lilichukuwa miezi kumi kujengwa na limepambwa kwa minara tisa, mwavuli mkubwa mweupe na sanamu za mbwa aliokuwa akiwapenda sana mfalme Bhumibol.

Kutakuwepo na maandamano mara sita kabla ya jeneza la mfalme huyo kupelekwa kwenye tanuu ya kuchomea maiti yake, liliojengwa karibu na kasri la mfalme. Hili ndiyo tukio kuu la msiba huo utakaodumu kwa siku tano. Mfalme Bhumibol ndiye alikuwa mfalme wa tisa wa himaya ya Chakri, ilioanzishwa katika eneo lililokuwa linaitwa Siam mwaka 1782.

Thailand Einäscherungszeremonie von König Bhumibol
Waombolezaji wakiwa wamekaa mbele ya tanuu la kuchomea mabaki ya mfalme Bhumibol, Alhamisi Oktoba 26,2017.Picha: picture alliance/AP Photo/W. Wanichakorn

Leo jioni katika sherehe iliogharimu dola milioni 90, waombolezaji wataonesha upendo wao katikati mwa Bangkok wakati wakishuhudia kile wanachoamini kuwa ni kurejea kwa roho ya mfalme huyo kwenye mlima wa mithiolojia wa Meru, ambao ndiyo kitovu cha kiroho cha Falme hiyo ya Kibudha.

Zaidi ya maua milioni 10 ya msandali yamekunjwa kwa ajili ya sherehe hiyo, kutokana na imani kwamba  harufu yake ni muongozo wa roho katika ulimwengu wa baada ya kifo.

Mwisho wa enzi

Licha ya mvua kunyesha majini Bangkok siku ya Jumatano, mamia kwa maelfu ya waombolezaji walipanga foreni kuchukuwa nafasi zao kuhsuhudia zoezi la uchomaji maiti. Jua limetoka leo Alhamisi na kundi la watu wapatao laki mbili na nusu wanatarajiwa, huku jamii nyingine za Thailand zikikusanyika katika mabanda mengi ya mfano yaliojengwa kote katika taifa hilo la Asia.

Maandamano na sherehe za msiba vitaonyeshwa pia katika vituo voyte vya televisheni nchini Thailand, ambapo vingi vimerekebisha rangi zake kwendana na rangi za msiba za nyeusi na njano.

Katika muda wa zaidi ya miongo saba aliokalia kiti cha ufalme, mfalme Bhumibol alisimamia mabadiliko yaliopelekea Thailand kuwa taifa la leyne uchumi wa kisasa na la utandawazi, huku likiwa na ufalme kama taasisi yake kuu.

Karibu familia 16 za kifalme na wawakilishi maalumu wanatarajiwa kuhudhuria sherehe kuu mjini Sanam Luang, akiwemo mwanamfalme wa Uingereza Andrew, malkia wa Uhispania Sofia, na rais wa zamani wa Ujerumani Christian Wulff.

Bhumibol Adulyadej Beisetzung Zeremonie Thailand
Mfalme wa sasa wa Thailand Maha vajiralongkorn akishiriki matembezi ya sherehe za mazishi ya baba yake Mfalme Bhumibol Adulyadej katika Kasri Kuu mjini Bangkok, Thailand, Oktoba 26,2017.Picha: Reuters/D.Sagolj

Mfalme mpya kurithi

Mtoto wa Mfalme Bhumibol mwenye umri wa miaka 65, mfalme Maha Vajiralongkom, atawasha kimbwi la msiba. Sherehe yake mwenyewe ya kutawazwa rasmi inatarajiwa kufuatia baada ya kuchomwa kwa mwili wa baba yake. Mwisho wa mwisho wa kifalme ulifanyika mwaka 1959 kwa kaka mkubwa wa hayati Bhumibol. Siku ya Ijumaa, majibu ya mfalme yatasafirishwa kwenda Kasri Kuu na katika Hekalu la Emerald Buddha.

Ukosoaji wa familia ya kifalme ni kosa kubw anchini Thailand na tangu taifa hilo liliporejea kwenye utawala wa kijeshi miaka mitatu iliyopita, jeshi limejionyesha kama mlinzi nambari moja wa taasisi ya ufalme.

Serikali ya kijeshi imewahamaisha watu kununua maua ya njano ili kuonyesha utiifu wao kwa hayati mfalme aliezaliwa siku ya Jumatatu, ambayo inahusishwa na rangi ya njano katika utamaduni na unajimu wa Thailand.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/afpe,dpae

Mhariri: Zainab Aziz