1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 100 waachiwa huru Congo

9 Machi 2017

Jeshi la Kongo limewaokoa watoto 100 ambao walizuiliwa kama wafungwa na wanamgambo katikati mwa nchi hiyo. Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchi Congo (MONUSCO).

https://p.dw.com/p/2YspA
DR Kongo MONUSCO Mission
Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini CongoPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Watoto, wenye umri wa miaka kati ya 4 na 16, waliachiwa  huru na jeshi baada ya mapanbano na wanamgambo wa Kamwena Nsapu kati ya Desemba 2016 na Mwaka 2017 Februari.

Kundi la hivi karibuni linalojumuisha watoto 20, akiwemo msichana mmoja, waliachiwa tarehe 23 Februari, alisema mwakilishi wa MONUSCO Charles Antoine Bambara, katika Mkutano wa waandishi wa habari kwenye mji mkuu - Kinshasa.

Inaaminika kuwa kundi la Kamwena Nsapu lilizilazimisha  au kuzishinikiza familia za watoto hao kuwatoa  ili watumike  kama majeshi. Baadhi yao walikuwa wanamgambo tangu Agosti 2016. Watoto hao walikuwa wakimiliki silaha mbali mbali kama vile visu, magongo na pia walifanya tambiko za kijadi wakiamini kuwa hawataathirika na chochote kile kitakachotokea vitani.

Wakati huo huo Makaburi  matatu ya halaiki yamegunduliwa eneo moja katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo mamia  ya watu wameuawa tangu Julai katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa ndani.

Kindersoldaten Jugendlicher mit einer AK-47 Uganda Sudan Lord's Resistance Army LRA
Mtoto aliyeingizwa katika kundi la wanamgambo wa Kamwena NsapaPicha: Getty Images/S.Price

Kwa mujibu wa  Umoja wa mataifa , watu wapatao 400 wameuwawa na 200,000 hawajulikani waliko, kutokana na mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa Kamuina Nsapu. Kiongozi wa kundi hilo Nsapu ambalo ni jina linalotumiwa na wapiganaji hao  aliuwawa, mwezi Agosti mwaka jana, katika mapigano kati ya jeshi na  wanamgambo, na mauaji hayo yalisababisha  ghasia kuongezeka  kwa haraka.

Umoja wa Mataifa inatana hatua ichukuliwe

Umoja wa Mataifa na vikundi vya haki, wakati huo huo, imelihutumu kundi hilo la Kamwena Nsapu kutumia watoto kuwa wanamgambo na kushambulia makanisa na majengo ya serikali.

Kongo 2003 Rebellen UPC
Mtoto katika kundi la wanamgamboPicha: AP

Vurugu za wanamgambo katika Jamhuri ya demokrasia ya Congo, zimezidisha migogoro ya ardhi, ukabila na  kugombania madini, na hali hiyo imezidi kuwa ngumu baada ya Rais Joseph Kabila kukataa kuachia madaraka yake  muda wake ulipomalizika

Desemba mwaka jana . Mamilioni ya watu walikufa katika vita , Mashariki ya nchi hiyo kutoka 1996-2003, na makundi kadhaa ya wanamgambo yanaendelea kuwepo karibu na mipaka ya Rwanda na Uganda, ingawa machafuko yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Uchunguzi rasmi wa Umoja wa mataifa uliofanywa eneo la kati nchi Congo, unahitaji kuchukuliwa hatua na makundi ya haki za binadamu au mabaraza la usalama kwa vile eneo hilo halimo katika sehemu ambako wachunguzi wa Umoja wa mataifa wana kibali kufanya uchunguzi wao.

Mwandishi : Najma Said

Mhariri : Mohamed Abdul- Rahman