1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watoto milioni 4 wahitaji msaada wa kitu Pakistan - UNICEF

25 Agosti 2023

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) linakadiria kwamba watoto milioni nne nchini Pakistan bado wanahitaji msaada wa kiutu na huduma muhimu mwaka mmoja baada ya mafuriko makubwa kuikumba nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4VZA0
Pakistan | Überschwemmungen in der Provinz Punjab
Picha: Rescue 1122 Emergency Department/AP Photo/picture alliance

UNICEF inasema uhaba wa fedha umekuwa kikwazo kikubwa katika kutekeleza majukumu yake.

Onyo hilo la UNICEF limekuja wakati mamlaka za Pakistan katika mkoa wa mashariki wa Punjab zinapambana kuwaokoa watu kutoka kwenye Mto Sutlej uliovunja kingo zake tangu Agosti Mosi.

Pakistan yaomba msaada wa kimataifa kufuatia mafuriko mabaya

Waokoaji wamefanikiwa kuwaokoa watu laki moja kutoka wilaya za Kasur na Bahawalpur.

Zaidi ya miezi sita baada ya mkutano ulioongozwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kusaidia kuijenga upya Pakistan baada ya mafuriko hayo, hakuna msaada ulioifikia nchi hiyo.

Mataifa na taasisi kadhaa za kimataifa ziliahidi kutoa dola bilioni 9 ila sehemu kubwa ya ahadi hizo ilikuwa ni mikopo au miradi ambayo bado iko katika awamu ya mipango.