1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndia

Watu 22 wauawa katika ajali ya boti India

Daniel Gakuba
8 Mei 2023

Ripoti rasmi zimearifu kuwa watu 22 wamekufa katika ajali ya boti ya utalii iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya 30 kusini mwa India.

https://p.dw.com/p/4R2MV
Picha ya maktaba ya ajali iliyofanyika oktoba 30, 2022 magharibi mwa Gujarat India.
Picha ya maktaba ya ajali iliyofanyika oktoba 30, 2022 magharibi mwa Gujarat India.Picha: Rajesh Ambaliya/AP Photo/picture alliance

Afisa wa polisi aliyetambulishwa kama Abdul Nazar amesema kuwa makundi ya waokoaji yanatarajia kupata miili zaidi kutoka ndani ya boti hiyo baada ya kuikokota kutoka kwenye mlango wa Mto Poorappuzha, karibu na mji wa Tanur.

Waziri wa michezo. V. Abdurahiman amesema miongoni mwa wahanga wamo watoto waliokuwa katika matembezi baada ya kumaliza muhula wa shule.

Wakati huo huo, watu wawili wameuawa katika jimbo la Rajasthan huko huko India, baada ya ndege ya kijeshi chapa MiG-21 kuanguka katika nyumba yao.

Jeshi la anga la India limesema rubani wa ndege hiyo yuko salama salimini.