1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 23,000 wamepotea kufuatia uvamizi wa Urusi, Ukraine

19 Februari 2024

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema hii leo kuwa inajaribu kufahamu ni kitu gani kilichowasibu watu wapatao 23,000 ambao wametoweka kufuatia machafuko ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4caJe
Rari la shirika la Msalaba Mwekunduz
Rari la shirika la Msalaba MwekunduPicha: Ashraf Amra/AA/picture alliance

Shirika hilo limesema linahitaji kubaini iwapo watu hao walitekwa, kuuawa au walipoteza mawasiliano baada ya kutoroka makwao. 

Muda mfupi baada ya uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari mwaka 2022, ICRC iliunda ofisi maalum ya ufuatiliaji iliyojitolea kuwatafuta wale waliopotea kutoka pande zote mbili kwenye mzozo huo.

Soma pia:Mashambulizi ya Urusi yaua takriban watu watatu katika miji ya mashariki mwa Ukraine

ICRC imesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, imepokea zaidi ya simu 115,000, maombi ya mtandaoni na hata barua kutoka kwa wanafamilia waliokata tamaa kutoka Urusi na Ukraine, ambao wanawasaka jamaa zao waliopotea.