1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 25 wauwawa Ukraine

Admin.WagnerD19 Februari 2014

Licha ya kuuawa kwa watu zaidi ya 20 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo mjini Kiev, waandamanaji wameapa kurudi kwenye Uwanja wa Uhuru kuendelea kushinikiza kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/1BBPZ
Ukraine Protest Eskalation und Gewalt 19.02.2014
moto unaowaka mjini KievPicha: Reuters

Rais Viktor Yanukovych huku rais huyo anawalalamikia viongozi wa upinzani kutokana na vurugu hizo kati ya polisi na waandamaji na kutishia kuchukua hatua kali zaidi.

Moshi, vilio na hasira ndiyo picha ya mji mkuu wa Ukraine, Kiev, asubuhi ya leo, baada ya vurugu zilizotekea jana, ambazo zinatajwa kuwa mbaya zaidi kutokea katika maandamano ya kupinga serikali ya Kiev, ambayo yamedumu kwa karibu miezi mitatu na kukwamisha shughuli mbalimbali mjini humo. Maelfu ya polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa na maguruneti na maji ya kuwasha waliwashambulia waandamanaji katika kambi yao mjini Kiev.

Mpinzani Klitschko aihimza maandamano

Kiew Proteste 18.02.2014
Kiongozi wa nchiki Ukraine Vitali KlitschkoPicha: Reuters

Kiongozi wa upinzani Vitali Klitschko amewataka waandamanaji kiasi cha 20,000 kwenda kuulinda uwanja wa Uhuru ambao umekuwa kitovu cha maandamano hayo, na ambao kwa sasa robo tatu inashikiliwa na polisi:

Kiongozi huyo ambae ni bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu aliwaambia waandamanaji kuwa hawataondoka katika eneo la kambi ya maandamano kwa kusema hicho ni kisiwa cha uhuru na watakilinda kwa kadiri wawezavyo.

Waandamanaji watoa kauli kali

Mapema leo wengi wa raia wameonekana kusikiliza wito wa kiongozi huyo. Mwanandamaji mmoja, Anthony Rybkovivich, mwenye umri wa miaka 32 amesikika akisema "Sitokwenda kukaa tu na kusubiri niuwawe, nakwenda kupambana."

Ukraine Protest Eskalation und Gewalt 19.02.2014
Idadi ya waandamanaji na polisi mjini KievPicha: Reuters

Kiasi ya watu 10,000 wameendelea kubakia katika uwanja huo wakati moto uliowashwa kwa kutumia matairi ukiendelea kuwaka. Jengo kubwa ambalo waandamanaji wamekuwa wakilitumia kama makao makuu limewaka moto na limetelekezwa wakati wa vurugu za usiku pale ambapo polisi walipotumia kipaza sauti kutangaza wanawake na watoto waondoke katika uwanja huo kwa kile walichosema kunafanyika operesheni ya kukabiliana na magaidi.

Upinzani walaumiwa kwa vurugu

Rais Yanukovych anasema viongozi wa upinzani wamevuuka mipaka kwa kutoa wito kwa watu kubeba silaha. Katika taarifa yake, kiongozi huyo ameutaka upinzani kujitenga na makundi ya wenye itikadi kali wanachochea vitendo vya umwagikaji damu na vurugu dhidi ya vikosi vya usalama.

Aidha Yanukovych aliongeza kusema kuwa endapo hawataondoka katika uwanja wa maandamano wataonekana kama wenye kuunga mkono misimamo ya wenye itikadi kali. Na kwa hivyo ameonya kwamba mazungumzo baina yao yanaweza kubadilika muelekeo wake.

Viongozi mbalimbali wa kimataifa wamepaza sauti zao juu ya hali ya mambo nchini Ukraine. Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden, ameonesha kusikitishwa kwake wakati alipozungumza na Yanukovych kwa njia ya simu. Huku sauti nyingine kutoka huko zikitoa wito wa taifa hilo kuwekewa vikwazo wazo ambalo limepingwa na Ujerumani.

Mwandishi: Sudi Mnette/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef