1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAustralia

Watu 5 wauawa mjini Sydney, Australia kwa shambulio la kisu

13 Aprili 2024

Mtu mwenye kisu amewashambulia na kuwauwa watu watano kwenye duka moja mjini Sydney nchini Australia leo, na kuwajeruhi wengine kadhaa.

https://p.dw.com/p/4eigA
Eneo mkasa wa shambulio la kisu ulipotokea mjini Sydney, Australia.
Eneo mkasa wa shambulio la kisu ulipotokea mjini Sydney, Australia.Picha: Steven Saphore/AP Photo/picture alliance

Polisi ya mji huo inasema mtu huyo, ambaye naye pia ameuawa, alianza kuwachoma watu visu ovyo ovyo, ambapo aliwapata tisa kati yao, kabla ya mwenyewe kupigwa risasi na polisi.

Mmoja kati ya waliojeruhiwa ni mtoto mdogo, kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Polisi Anthony Cooke. Polisi inasema mshambuliaji huyo alifanya tukio hilo peke yake na hakukuwa na kitisho cha kuendelea kwa mashammbulizi hayo.

Hadi sasa, maafisa hawajataja utambulisho wa mshambuliaji huyo, na wala dhamira ya shambulio hilo. Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema amefadhaishwa na mkasa huo na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za walipoteza maisha.