1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu karibu 100 wauwawa Syria

17 Agosti 2015

Idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya anga katika mji unaoshikiliwa na waasi nje ya Damascus inakaribia kufikia 100, wakati kiongozi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la kibinadamu akiwa na hofu kubwa

https://p.dw.com/p/1GGs0
Mashambulizi ya angani SyriaPicha: picture alliance/abaca

Mfululizo wa mashambulizi ya jana katika mji wa Douma katika ngome ya waasi ya mashariki mwa Ghouta yalikuwa ni moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya umwagaji damu katika kipindi cha miaka minne cha vita nchini humo.

Mashmbulizi hayo yanakuja ikiwa ni karibu miaka miwili kupita baada ya mashambulizi ya kutumia silaha za sumu katika eneo hilo hilo ambayo pia jumuiya ya kimataifa ilielekeza lawama zake kwa serikali ya Syria.

Upinzani walaani mauwaji

Muungano mkuu wa upinzani nchini Syria uliopo uhamishoni kililaani mashambulizi yote hayo na mrejesho kidogo unaotokana na huduma inayotolewa kwa majeruhi waliotokana na mashambulizi hayo.

Mitglieder der palästinensischen Familie von Saad Dawabsha
familia iliyofikwa na mkasa DoumaPicha: picture-alliance/dpa/Stringer

Karibu watu 96 waliuawa katika mashambulizi hayo kumi ya anga yaliyotokea katika eneo la soko ikiwa ni kwa mujibu wa chombo cha waangalizi wa haki za binadamu cha Syria chenye masikani yake nchini Uingereza.

Kiasi cha watu wengine 240 walijeruhiwa katika tukio hilo na idadi ya vifo vinazidi kuongezeka miongoni mwa majeruhi waliokuwa na hali mbaya zaidi.

Kiongozi mkuu wa waangalizi hao wa haki za binadamu Rami Abdel Rahman alisema ndege za kivita za serikali zilifanya mashambulizi mengine manne katika mji wa Douma hii leo asubuhi lakini hakuwa na taarifa za haraka kuhusiana na idadi ya majeruhi wa tukio hilo.

Mpiga picha wa shirika la habari la AFP aliyaelezea mashambulizi hayo kama moja ya mashambulizi mabaya zaidi aliyowahi kuyashuhudia kwenye mji huo katika kipindi chake cha utendaji kazi.

Anasema aliona miili mingi ya watu ikiwa imelazwa katika sakafu iliyotapakaa damu ktika wodi moja wapo ya wagonjwa mjini Douma mnamo wakati madaktari wakijitahidi kutoa huduma ya matibabu kwa wahanga wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa mpiga picha huyo wakazi wa mji huo mapema jumatatu walianza kuzika maiti zilizotokana na mashambulizi hayo.

Wachimba kaburi katika eneo hilo wanalazimika kuchimba kaburi kuibwa litakalo tosha kuzika idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha.

Mji wa mashariki wa Ghouta ambao ni ngome kuu ya waasi umekuwa mara kwa mara katika msukosuko ukilengwa na ndege za kivita za serikali na ukiwa umezingirwa katika kipindi cha miaka miwili sasa.

Wakati huo huo mataifa ya Urusi na Iran yamesema makundi mbalimbali nchini Syria likiwemo kundi pinzani yanapaswa kuamua juu ya hatima ya Rais Bashar al Assad huku Urusi ikipinga mazungumzo yoyote ya mapema yatakayolenga kuondolewa kwa Rais Assad madarakani kama moja ya hatua ya kufikia makubaliano ya amani.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Ravrov na mwenzake wa Iran, Mohamed Javad Zarif walitetea hatua ya mataifa yao ya kumuunga mkono Assad katika mgogoro huo ambao tayari umeua karibu robo ya watu millioni tangu mwaka 2011.

Vikundi vya upinzani nchini Syria , mataifa yaliyoko katika ghuba ya kiarabu na nchi za magharibi yanataka kuondolewa madarakani kwa Rais Assad.

Mwandishi: Isaac Gamba/ AFPE/RTRE
Mhariri: Iddi Ssessanga