1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu waliokamtwa Berlin sio washukiwa wanaotafutwa wa RAF

3 Machi 2024

Polisi ya sema watu wawili waliokamatwa katika msako wa wanaoshukiwa kuwa ni magaidi wa kikundi cha mrengo wa kushoto cha Red Army Faction RAF, sio washukiwa Ernst-Volker Staub na Burkhard Garweg.

https://p.dw.com/p/4d7NX
Polisi ya Ujerumani yawasaka magaidi wa kikundi cha mrengo wa kushoto cha Red Army Faction RAF
Polisi ya Ujerumani yawasaka magaidi wa kikundi cha mrengo wa kushoto cha Red Army Faction RAFPicha: picture alliance/dpa

Kulingana na msemaji wa Polisi katika Jimbo la Saxony, Ulrike Trumtar, polisi walifanya msako katika mji wa Berlin mapema leo Jumapili wakiwasaka washukiwa hao kwa madai ya ugaidi na wamekuwa mafichoni  kwa miongo kadhaa iliyopita.

Milio ya risasi ilisikika katika eneo la tukio lakini hakuna majeruhi walioripotiwa. Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini iwapo watu wawili waliokamatwa leo wana uhusiano na kundi la RAF.

Katika miaka ya 1970 na 1980, RAF ilifanya mfululizo wa mashambulizi Ujerumani Magharibi wakati huo kupitia mashambulizi na utekaji nyara, huku jumla ya mauaji zaidi ya 30 yakihusishwa na kundi hilo. 

Hata hivyo RAF ilisambaratishwa mnamo1998 na hakuna ushahidi kwamba kundi hilo la zamani la kigaidi bado linafanya kazi.