1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Watu wanakufa njaa huko Gaza lasema shirika la WFP

9 Desemba 2023

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema uwezo wa ugawaji wa mahitaji ya kimsingi kwa raia katika ukanda wa Gaza uko katika hatari ya kuvurugika wakati vita vikiendelea.

https://p.dw.com/p/4ZxtN
Shirika la WFP limesema uwezo wa ugawaji wa mahitaji ya kimsingi kwa raia katika ukanda wa Gaza uko katika hatari
Shirika la WFP limesema uwezo wa ugawaji wa mahitaji ya kimsingi kwa raia katika ukanda wa Gaza uko katika hatariPicha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/picture alliance

Kupitia mtandao wa kijamii wa X Naibu Mkurugenzi wa WFP Carl Skau amesema kwamba hakuna chakula cha kutosha na watu wanakufa njaa.

Skau ameandika kwamba maelfu ya watu waliokata tamaa na wenye njaa wamejazana katika vituo vya usambazaji wa misaada ya kibinadamu, makazi ya dharura, kambi na vyoo vimejaa na kutolewa wito usitishwaji mapigano.

Huku haya yakijiri jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo kadhaa ya Hezbollah nchini Lebanon.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, ambayo zamani ilikuwa Twitter, jeshi la Israel IDF limesema kwamba ndege zake za kivita zilishambulia maeneo ya Hezbollah kwenye mpaka wake wa kaskazini.

Hezbollah, kundi linaloungwa mkono na Iran, limetajwa kama shirika la kigaidi na Umoja wa Ulaya, Marekani na Israel, na limeonyesha ushirikiano kwa kundi la  Hamas katika vita dhidi ya Israel, ingawa makundi hayo mawili yana maslahi tofauti, huku Hezbollah ikizingatia zaidi jukumu lake nchini Lebanon na Syria.