1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Lebanon akosoa uchochezi wa Israel mpakani

Iddi Ssessanga
28 Julai 2020

Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab amesema Israel imekiuka mamlaka ya taifa lake kwa uchochezi hatari wa kijeshi kwenye mpaka kati ya mataifa hayo na kutoa wito wa tahdhari baada ya kuongezeka kwa mzozo wa mpakani.

https://p.dw.com/p/3g2vv
Israel Libanon | Konflikte an der Nordgrenze
Picha: AFP/J. Marey

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema vikosi vya nchi yake vilizuwia jaribio la kundi la Kishia la Lebanon la Kishia linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah, kujipenyeza nchini Israel kupitia mpaka wa Lebanon Jumatatu, madai ambayo yamekanusha na Hezbollah.

Makabiliano ya mpakani ambayo Israel ilisema yalihusisha majibizano ya risasi kati ya vikosi vyake na watu wenye silaha, yalifuatia siku kadhaa za kuongezeka kwa mzozo kati ya Hezbollah na taifa hilo la Kiyahudi.

Waziri Mkuu Netanyahu alisema Hezbollah ilikuwa incheza na moto, na kusisitiza kuwa kundi hilo na serikali ya Lebanon wabebe dhamana ya jaribio la wapiganaji kujupenyeza kwenye ardhi yake, na kusababisha makabiliano hayo.

"Tunachukulia kwa uzito jaribio hili la kujipenyeza katika ardhi yetu. Hezbollah na Lebanon zinawajibika kikamilifu kwa tukio hili na shambulio lolote kutoka ardhi ya Lebanon dhidi ya Israel. Shambulio lolote dhidi yetu litajibiwa kwa nguvu kubwa", alisema Netanyahu katika mkutano na waandishi habari.

Israel Jerusalem | Coronavirus | Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Picha: picture-alliance/dpa/G. Tibbon

Hezbollah yakanusha kuhusika

Jeshi la Israel lilisema kundi la wanaume watano waliojihami kwa bunduki za mashambulizi walivuka msitari wa Blu unaozitenganisha Israel na Lebanon katika eneo linalozozaniwa la Mlima Dov, ambalo linadaiwa na Lebanon, Syria na Israel kuwa la kwao.

"Kundi hilo lilivuka msitati wa Blu kuelekea Israel, vikosi vya ulinzi vya Israel viliwafyatulia risasi na kuharibu mipango yao. Hakukuwa na majeruhi kati ya vikosi vyote.

Vikosi vya ulinzi vya Israel vitachukuwa tahadhari ya juu na vitandelea kufanya kazi yake kulingana na mahitji. Hatutaruhusu ukiukaji wa mamlaka ya Israel au uhuru wa watu wake," alisema Avichay Adraee, msemaji wa jeshi la Israel.

Lakini Hezbollah, ambayo ina uwepo katika eneo ambako tukio hilo lilitokea, ilikanusha ushiriki wowote. Ilisema kwamba ripoti za Israel kutibua njama ya kujipenyeza kutoka Lebanon ni za "uongo mtupu."

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa UNIFIL, umesema umeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Libanon TV-Ansprache von Ministerpräsident Hassan Diab
Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan DiabPicha: AFP/DALATI AND NOHRA

Waziri Mkuu Diab atoa wito wa tahadhari

Lakini waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab alisema kupitia ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba Israel imekiuka mamlaka ya Labanon kwa mara nyingine.. katika uchochezi hatari wa kijeshi. Hili ndiyo lilikuwa tamko la kwanza rasmi la serikali yake kufuatia mashambulizi hayo ya Jumatatu.

"Natoa wito wa kuchukuwa tahdhari katika siku zijazo, kwa sababu nahofia mambo yatakuwa mabaya zaidi kwa kuzingatia mzozo wa mpakani," alisema waziri mkuu huyo.

Diab ameishutumu Israel kwa kujaribu kubadili sheria za vita zilizokuwepo kati ya mataifa hayo mawili tangu kumalizika kwa vita vilivyodumu mwezi mzima mwaka 2006 - ambavyo ndiyo vilikuwa mzozo wa mwisho wa moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili.

Amesema pia Israel inajaribu kubadili mamlaka ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa UNIFIL, kabla ya kumalizika muda wake mwezi ujao.

Malumbano kuhusu mamlaka ya UNIFIL

Mwanzoni mwa mwezi Mei, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Kelly Craft, alitoa wito kwa chombo hicho cha dunia, "kufanya mabadiliko makubwa kuiwezesha UNIFIL au kufanya marekebisho ya watumishi wake na rasilimali," kwa sababu ujumbe huo ulikuwa "unazuwiwa kutekeleza majukumu yake."

Sayyed Hassan Nasrallah Hisbollah-Chef
kiongozi wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah.Picha: picture-alliance/dpa/N. Mounzer

Kiongozi wa Hezbollah Hassan NAsrallah alipinga amra moja pendekezo hilo ambalo alisema lilikuwa takwa la Israel. Tukio la karibuni la mpakani linafuatia shambulio la kombora la Israel Julai 20 dhidi ya ngome za serikali ya Syria kusini mwa Damascus, ambalo liliuwa watu watano.

Hezbollah, ambalo wapiganaji wake wanaiunga mkono serikali ya Damascus katika vita vyake vya miaka tisa dhidi ya waasi, lilisema moja wa wanachama wake alikuwa miongoni mwa waliouawa.

Tangu mwaka 2011, Israel imefanya mamia ya mashambulizi nchini Syria, ikivilenga vikosi vya serikali na vikosi washirika vya Iran na Hezbollah, kwa lengo inalolitaja kuwa kukomesha uwepo wa kijeshi wa iran nchini Syria.

Chanzo: Mashirika