1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu mpya wa Kosovo aidhinishwa rasmi

10 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/CnG8

PRISTINA

Bunge la jimbo la Kosovo lililojitenga na Serbia limeidhinisha serikali yake mpya inayoongozwa na waziri mkuu Hashim Thaci.Serikali hiyo mpya ya mseto kati ya chama cha waziri mkuu Thaci na kile cha mpinzani wake mkuu cha Demoktratic League of Kosovo inatazamiwa kuliongoza jimbo la Kosovo kuelekea kujitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia katika muda wa wiki chache zijazo.Serbia ambayo itafanya uchaguzi war ais mwezi huu inapinga vikali pendekezo hilo la Kosovo kujitangazia uhuru.Wakati huohuo tume ya Umoja wa Ulaya imesema matumaini ya Serbia ya kusaini makubaliano muhimu ya kibiashara na msaada pamoja na Umoja huo hayategemei hatma ya jimbo hilo la Kosovo.