1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Ethiopia aanza muhula wa pili madarakani

Mohammed Khelef
5 Oktoba 2021

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ameanza muhula wake wake pili madarakani akikiri kwamba vita kwenye jimbo la kaskazini la Tigray vinaigharimu vibaya sana nchi yake.

https://p.dw.com/p/41Gwg
Äthiopien | Vereidigung Abiy Ahmed
Picha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Abiy aliapishwa jana mbele ya viongozi kadhaa wa Afrika waliohudhuria hafla hiyo jijini Addis Ababa. Miongoni mwa waliohudhuria ni viongozi wa Nigeria, Senegal, Uganda, Somalia, Djibouti, Kenya na Sudan Kusini. Eritrea iliwakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeni.

Aliuambia umati kwenye sherehe hiyo kwamba mgogoro wa Tigray umeifanya Ethiopia kulipa gharama kubwa.

Amesema katika jumuiya ya kimataifa kuna wale ambao wameonesha urafiki na ambao wamewasaliti.

Chama cha Ustawi chake Abiy Ahmed kilitangazwa mshindi wa uchaguzi wa bunge uliofanyika mapema mwaka huu, licha ya uchaguzi huo kususiwa na kukoselewa na wapinzani, ingawa ukisifiwa na waangalizi kama ulioratibiwa vyema zaidi kuliko chaguzi zilizotangulia.