1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Sudan aapishwa rais wa mpito

Lilian Mtono
12 Aprili 2019

Waziri wa ulinzi wa Sudan Awadh Ibn Auf ameapishwa kuwa rais wa baraza la mpito la kijeshi ambalo kulingana na jeshi litaongoza kwa kipindi cha miaka miwili ya mpito.

https://p.dw.com/p/3Ge1l
Sudan | Awad Ibn Auf als Präsident des militärischen Übergangsrates vereidigt
Picha: picture-alliance/AA

Kituo cha radio kinachomilikiwa na serikali kimearifu kuwa mkuu wa majeshi Kamal Andel-Marouf ameapishwa kuwa makamu wa rais wa baraza hilo.

Hatua hii imekuja huku waandamanaji wakilalamika kwamba utawala huo wa kijeshi haukumaanisha mabadiliko, na kuahidi kuendelea kuandamana hata baada ya hapo jana kutangazwa kwa sheria inayozuia raia kutembea usiku wa kuanzia saa 4 hadi saa 10 alfajiri.

Rais Omar al Bashir wa Sudan aliyetawala kwa miaka 30, jana Alhamisi alipinduliwa na kukamatwa kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali. Rais Omar al-Bashir aliyetawala Sudan kwa miaka 30 amepinduliwa na kukamatwa baada ya miezi kadhaa ya maandamano makubwa yaliyoipinga serikali.

Sudan Omar Al-Bashir
Omar al-Bashir ameongoza Sudan kwa miaka 30. Bashir pia anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC.Picha: Reuters/M. N. Abdallah

Upinzani na raia hawana imani na mapinduzi hayo.

Makundi ya upinzani nchini humo yametoa mwito kwa waandamanaji kusalia mitaani wakipinga mapinduzi hayo ya kijeshi. Kundi hilo lililozungumza kwa niaba ya waratibu wa maandamano hayo wamesema kwenye taarifa yao kwamba mapinduzi pamoja na kusimikwa kwa utawala wa kijeshi wa mpito kwa namna yoyote hakukuashiria mabadiliko. 

Waandamanaji waliendelea kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ikiwa ni siku ya sita mfululizo, wakati sheria iliyotangazwa na jeshi ya kutotembea nje kuanzia majira ya saa 4 za usiku ikiwa imeanza kutekelezwa nchini humo, licha ya kuongezeka kwa mbinyo wa jamii ya kimataifa dhidi ya jeshi wakitaka wakabidhi madaraka kwa raia. Awali jeshi liliwaonya raia kutopuuza tangazo hilo.

Umoja wa Ulaya ameliomba jeshi la Sudan kufanya mabadilishano hayo ya madaraka haraka. Mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Federica Mogherini amesema mchakato wa siasa wa kuaminika na jumuishi ndio pekee utakaofanikisha kufikiwa kwa matarajio ya watu wa Sudan.   

Msemaji wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, Guterres ametoa mwito wa mabadilishano yatakayokidhi matarajio ya kidemokrasia miongoni mwa watu wa Sudan.

Baadhi ya raia wa Sudan wamezungumzia mapinduzi hayo kwa mshituko na fadhaa. Walichokifanya raia walioandamana kupinga utawala wa kifisadi ni sawa na kuruka majivu na kukanyaga moto.