1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung atembelea kikosi cha wanamaji wa Ujerumani huko Djibouti

Christoph Grabenhainrich/Mohamed Dahman22 Desemba 2008

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung leo hii ametembelea kikosi cha wanamaji cha Ujerumani huko Djibouti.

https://p.dw.com/p/GLTM
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung.Picha: EUROFORUM/Hergenröder

Kuanzia huko ndipo manowari ya Ujerumani inayoitwa Karlsruhe itafunga safari hapo kesho kuelekea fukwe za Somalia kujiunga na operesheni ya Atalanta ya Umoja wa Ulaya kupambana na maharamia.

Repoti ya mwandishi wa Deutsche Welle Christoph Grabenheinrich imelenga ziara ya waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani.

Kutokana na ziara hiyo fupi ya waziri wa ulinnzi wa Ujerumani Franz Joseph Jung wa chama cha CDU fuko lililojaa zawadi kwa mabaharia wa manowari ya Karlsruhe analowapelekea inabidi tusubiri tutambuwe.Kwa hiyo matarajio na masuali ya wazi zaidi yanamsubiri waziri huyo.Ukweli ni kwamba kuna haja ya kutumwa kwa vikosi vya majini vya Ujerumani kupambana na maharamia kwenye Pembe ya Afrika. Ulrich Kirsch ni mkuu wa shirikisho la vikosi vya Ujerumani.

Kirsch amesema kikosi hicho cha wanamajai kina mamlaka yenye nguvu ambapo ufafanuzi wa utekelezaji wake ni siri inayoshikiliwa na wizara.Mamlaka waliyopewa na serikali wanaruhusiwa katika hali mbaya sana kuchukuwa hatua hii lakini kiini cha dhamira yenyewe sio kuwasaka maharamia zaidi ni kuwatisha maharamia hawa.

Ikiwa hakuna njia nyengine yaani inapolazimika vikosi hivyo vinaruhusiwa kuzamisha meli za maharamia na kukombowa meli iliyotekwa nyara hivyo ndivyo anavyosema waziri wa ulinzi wa Ujerumani Frank Joseph Yung.

Anasema dhamira ni kujihami na mashambulizi lakini ikitokea hali kama hiyo kikosi chao cha wanamaji pia kina zana ya kukabliana na hali hiyo.Kwa hiyo wana kikosi maalum kilichopatiwa mafunzo maalum kwa ajili ya hali hiyo ili kwamba pia waweze kuchukuwa hatua kukabiliana na hali kama hiyo.

Jukumu kuu la manowari za Ujerumani litakuwa ni kusindikiza meli zinazobeba misaada ya chakula ya Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa pamoja na meli nyengine za mizigo.Hata hivyo wale wanaokosowa operesheni hiyo wanasema operesheni hiyo Atalanta yenye meli za kivita sita na ndege tatu za upelelezi ni operesheni yenye umbo la kiishara tu.Lakini kwa vyo vyote vile Reinhold Robbe anayeshughulikia masuala ya jeshi la Ujerumani bungeni wa chama cha SPD anafikri angalau operesheni hiyo Atalanta itakuwa na mafanikio ya kisaikolojia.

Robbe anafikiri hilo ni jambo zuri kwamba kule kuwepo pekee kwa manowari za kivita kutawatia hofu maharamia.

Kwa upande mwengine serikali inategemea ufumbuzi wa kimataifa kwa suala hilo kama hapa anavyosema waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir.

Kwa mujibu wa Steinmeir Umoja wa Ulaya unafuatilia kufikia makubaliano na mataifa mengine iwapo maharamia wanakamatwa waweze kufikishwa mahkamani katika nchi hizo nyengine.

Mafanikio ya operesheni Atalanta hayawezi kupatikana hivi karibuni kwa kuzingatia kwamba kwa miaka 15 jumuiya ya kimataifa imekuwa ikishuhudia kusambaratika kwa Somalia bila ya kuchukuwa hatua yoyote ile.