1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wiki ya maonesho ya kilimo yaanza mjini Berlin.

Sekione Kitojo15 Januari 2009

Maonyesho ya bidhaa za kilimo yanaanza leo mjini Berlin, ambapo waonyeshaji bidhaa karibu 1,600 kutoka nchi 56 wanashiriki kuonesha bidhaa zao.

https://p.dw.com/p/GZGa
Watu mbali mbali wakiwa katika tamasha wakati wa ufunguzi wa maonesho ya wiki ya kilimo mjini Berlin siku ya Alhamis wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo.Picha: AP

Waonyeshaji bidhaa 1,600 kutoka nchi 56 duniani , pamoja na watazamaji karibu ya 400,000 wanatarajiwa kutembelea maonyesho ya wiki ya kilimo yanayoanza leo Ijumaa kukitarajiwa na msongamano mkubwa, huku watayarishaji hata hivyo wakiwa na hisia tofauti katika maonyesho hayo makubwa ya kilimo duniani.



Makampuni ya kilimo na yale yanayozalisha bidhaa za kilimo yanahisi kuwamo katika mzozo wa kiuchumi, lakini hata hivyo yameonyesha wiki hii kuwa yana matumaini kwa mwaka huu 2009.

Kutokana na maonyesho haya mwanzoni mwa mwaka huu yanataka kuonyesha vipi sekta hii inavyoweza kufanikiwa. Hadi tarehe 25 Januari ,wiki ya kilimo patakuwa panaonyeshwa mbinu mpya pamoja na zile zilizokwisha tumika ikiwa pia ni pamoja na njia ya kukupatia nguvu zaidi kwa kukupa burudani kutoka duniani kote. Ufunguzi rasmi umefanyika jana Alhamis kwa tamasha kubwa.

Maonyesho hayo pia ni sehemu ya wanasiasa kutoka duniani kote kukutana , ambapo pekee mawaziri 30 wa kilimo watajumuika katika ukumbi pamoja na mnara wa radio pamoja na katika maeneo ya kutoa maelezo kwa waandishi wa habari.

Serikali ya Ujerumani inataka wiki hii ya kilimo kuwa kama mkusanyiko wa Davos kwa upande wa kilimo, ikiwa mfano wa jukwaa la dunia la uchumi linalofanyika kila mwaka katika mji wa Davos nchini Uswisi.

Waziri wa kilimo wa Ujerumani, Ilse Aigner, kutoka chama cha CSU, atajadili pamoja na wenzake kuhusu mzozo wa chakula pamoja na mzozo uliofuata wa kiuchumi. Waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin, anapanga kuhudhuria maonyesho hayo pia.

Kulikuwa na mbinyo kutoka kwa wafugaji wanaozalisha maziwa kabla ya maonyesho hayo, wametishia kutokana na kupungua kwa bei ya maziwa kuzuwia ugavi wa maziwa. Tunawapa wanasiasa muda , kuondoa mkwamo huu. Iwapo hilo halitatokea, wamesema wafungaji hao wa ng'ombe , ni dhahiri kuwa tutafikiria kufanya mgomo wa kutoa maziwa, amesema Romuald Schaber, rais wa chama cha wazalishaji maziwa nchini Ujerumani.

Chama hicho mwezi Mei na Juni mwaka 2008 kilifanya mgomo wa kusambaza maziwa nchini Ujerumani kwa muda wa siku kumi, wakidai bei ya juu ya bidhaa hiyo.

Kuhusiana na mzozo wa uchumi, amesema rais wa chama cha wakulima nchini Ujerumani Gerd Sonneleitner, kuwa wakulima watakuwa wameharibikiwa.

Tunazalisha chakula , ambacho kinahitajika pia katika kuinua uchumi. Mzozo wa aina hiyo hauwezi kupita bila kuonekana katika suala la uchumi, amesema waziri wa kilimo Aigner. Kilimo cha Ujerumani kiko katika hali ya uimara, hali ambayo inaonekana pia katika masoko.

Chama cha makampuni ya Ujerumani yanayotengeneza chakula kinazungumzia matumaini pia katika mwaka huu 2009. Kutokana na mzozo wa kiuchumi mwaka 2009 utakuwa mwaka wenye nafuu katika uwezekano wa ukuaji wa uchumi, amesema mwenyekiti wa chama hicho Jürgen Abraham. Usafirishaji nje bidhaa utaendelea kukua, lakini hapa nchini hali itapungua kidogo, kwa kuwa wateja hawataweza kununua. Kupanda kwa bei ya vyakula inapaswa kusitishwa, na kutokana na changamoto hiyo, wateja nchini Ujerumani hawapaswi kuingia zaidi katika mifuko yao na kutumia zaidi amesema Abraham.