1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kwa serikali ya Kenya

John Marwa29 Aprili 2015

Wanaharakati wa kutetea haki za walemavu mjini Kisumu wametoa wito kwa serikali ya Kenya kuongeza juhudi za kukabiliana na changamoto zinazowakumba walemavu wa ngozi.

https://p.dw.com/p/1FHQu
Mlemavu wa ngozi Leondiah pamoja na jamaa yake mmoja nchini Kenya
Picha: DW/G. Ketels

Wakizungumza na DW mjini humo wamesema inasikitisha kuona kwamba hakuna hatua zozote za tahadhari zilizotangazwa na serikali, licha ya vitendo vya kutekwa na kuuawa kwa walemavu wa ngozi kuongezeka katika nchi jirani ya Tanzania. Kusikiliza ripoti ya mwandishi wetu John Marwa, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman