1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

Hamidou, Oumilkher22 Januari 2008

Vurugu katika masoko ya hisa ndio mada iliyohanikiza magazetini nchini Ujerumani hii leo

https://p.dw.com/p/CvtI
Bunge la Indonesia lazungumzia vurugu katika soko la hisa mjini JakartaPicha: picture-alliance / dpa



Magazeti takriban yote ya Ujerumani yamezungumzia hii leo kwa mapana na marefu juu ya vurugu katika masoko ya hisa.Hata hivyo uchaguzi wa rais nchini Serbia nao pia haukusahauliwa.


Tuanze basi na vurugu katika masoko ya hisa kote ulimwenguni-vurugu lililopelekea hisa kuporomoka vibaya sana.Faharasa ya Ujerumani-Deutsche Aktienindex-DAX imeporomoka vibaya sana-hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu september 11 mwaka 2001-imepoteza zaidi ya asili mia sabaa masoko ya hisa yalipofungwa.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:



 Kuporomoka vibaya sana kima cha thamani katika soko la hisa la Ujerumani kumevuruga matumaini ya miezi kadhaa kuona soko la hisa la Ujerumani likinusirika na hali jumla namna ilivyo katika masoko ya fedha na kuzidisha nguvu za hisa za Ujerumani dhidi ya zile za Marekani au hata  za nchi nyengine za Ulaya.Maarifa yametuonyesha kwamba mtafaruku katika masoko ya hisa mara nyingi hufuatwa na nafuu.Kama nafuu hiyo itakua ya muda mrefu-hilo ni suala jengine.Kwasababu uwezekano upo kuiona hali ya mambo katika nchi tajiri kiviwanda ikizidi kuwa mbaya.Kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba mkondo wa mambo katika masoko ya hisa ya kimataifa utaendelea kushawishiwa na hali ya mambo nchini Marekani.Sababu ya kuzuka vurugu katika masoko ya hisa hakuna kwasasa, lakini hata sababu ya mtu kujipa na matumaini haiko pia.



"Kwa bahati mbaya hakuna mabadiliko yoyote ya maana yanayotegemewa baada ya mzozo huu wa masoko ya hisa" analalamika mhariri wa gazeti la mjini Berlin TAGESZEITUNG anaendelea kuandika:



"Wahakiki tangu wa ndani mpaka wa nje ya ulimwengu wa fedha hawana nguvu zozote.Hawajafanikiwa hata katika nchi moja ya kiviwanda kushawishi sera za serikali kuhusiana na suala hilo.Ili kuleta wezani sawa kati ya masilahi ya wanaviwanda na yale ya jamii,panahitajika mkakati wa muda mrefu wa kisiasa.Mbinu za kukadiria mambo zinabidi zidurusiwe hatua baada ya hatua ili kuepukana na biashara ya kubahatisha katika masoko ya hisa- na kuhimiza pawepo hali ya uwazi-Hakuna lolote  kati ya hayo litakalotekelezwa-linalalamika gazeti la TAZ.



Mada ya pili magazetini inahusu uchaguzi wa rais nchini Serbia.Mgombea anaefuata siasa kali za kizalendo NIKOLIC amejikingia kura nyingi zaidi katika duru ya kwanza kumpita mtetezi wa kiti cha rais,TADIC.Gazeti la FRANKFUERTER ALLGEMEINER linasema Umoja wa Ulaya unapima kwa jinsi gani unaweza kumsaidia Tadic.Gazeti linaendelea kuandikla:



 "Kuna fikra mbili zinazojitokeza:ya kwanza Umoja wa Ulaya ungeweza kutia saini,muda mfupi kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais kuitishwa,makubaliano ya ushirikiano pamoja na Serbia-jambo ambalo litamsaidia sana Tadic.Zaidi ya hayo Umoja wa Ulaya ungebidi ufikirie uwezekano wa kuondowa vizuwizi vya kupatiwa viza waserbia.Fikra hii pia ni sawa.Kwasababu wahalifu wa kiserbia hawatakosa njia ya kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya-vizuwizi vya viza viwekwe au viondolewe.Kila mserbia lakini anaetaka kujionelea mwenyewe kama kweli nchi za magharibi ziko kama wanavyoambiwa na wanasiasa wanaofuata siasa kali,anashindwa mara nyingi kutokana na vizuwizi vya Schengen.Kwa namna hiyo nchini Serbia kuna kizazi kilichotengwa ambacho Ulaya wanaisikia tuu-mfano kutoka kwa mpigania siasa kali za kizalendo Nikolic.