1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON: Juhudi za upatanisho nchini Myanmar

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLb

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari amewasili nchini Myanmar kuzungumza na viongozi wa kijeshi waliotumia nguvu kupambana na maandamano.Gambari baada ya kuwasili Yangon moja kwa moja alikwenda Naypyidaw kukutana na viongozi wa kijeshi wanaotawala nchini Myanmar.Mji huo ulio kama kilomita 300 kaskazini ya Yangon ulitangazwa na utawala wa kijeshi kama makao makuu ya serikali ya Myanmar,nchi inayojulikana kama Burma pia.