1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wakabiliwa na utapiamlo Yemen

27 Oktoba 2020

Utapiamlo miongoni mwa watoto wadogo umeongezeka kwa viwango vya juu kabisa kuwahi kurekodiwa katika sehemu za Yemen, eneo ambalo limegubikwa na vita wa muda mrefu sasa.

https://p.dw.com/p/3kUpA
Jemen Kinder im Flüchtlingslager in der Provinz Hajjah
Picha: picture-alliance/Photoshot/M. Al Wafi

Taarifa kutoka Umoja mataifa zinasema, Yemen ipo katika hali ngumu wakati huu wa janga la Corona na upungufu katika ufadhili wa msaada unazidisha mzozo wa kibinadamu.

Takwimu zinaashiria kuwa zaidi ya visa nusu milioni vya viwango vya juu utapiamlo kati ya watoto chini ya miaka mitano vimerekodiwa kusini kwa nchi hiyo huku takwimu kutoka maeneo ya kaskazini zikiendelea kuratibiwa lakini kuna matarajio kuwa hali itakuwa kama ilivyo kusini mwa Yemen

Soma zaidi:Yemen na kitisho kipya cha njaa

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya shirika la Chakula na kilimo, Shirika la mpango wa chakula na Umoja Mataifa kitengo cha kushughulikia maswala ya watoto UNICEF asilimia 15.5 ya visa hivyo vimewaacha takriban watu 98,000 katika hatari ya kufariki iwapo hawatapokea matibabu ya haraka.

Jemen Darwan Flüchtlingslager
Mtu ameketi mbele ya hema katika kambi ya wakimbizi ya DarwanPicha: picture-alliance/AA/M. Hamoud

"Takwimu wanazotoa  zinathibitisha kuwa utapiamlo mkali miongoni mwa watoto umefikia viwango vya juu zaidi tangu kuanza kwa vita nchini humo," amesema Lise Grande, mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja Matiafa Yemen.

Janga la COVID-19 limeongeza kadhia ya Yemen

Yemen imegubikwa na vita tangu mwaka 2014, kati ya kundi la waasi wa Kihouthi linaloungwa mkono na Iran, na serikali iliyovunjika ambayo inaungwa mkono na muungano wa kijeshi Saudia na kuizamisha Yemen katika mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu.

Aidha Umoja Mataifa umedokeza kuwa kuongezeka kwa mzozo na kupungua kwa uchumi, pamoja na athari kubwa ya janga la Covid -19, kumeongeza kadhia ya Wayemen kufikia ukingoni, huku mipango ya misaada pamoja na misaada wa dharura ya chakula kuvurugika kutokana na ukosefu wa fedha.

Lisa Grande
Picha: picture-alliance/AA/Y. Keles

Yemen inahitaji Dola bilioni 3.2 kukabiliana na tatizo hilo na kufikia mwezi Oktoba imepokea Dola bilioni 1.43 pekee.

Mwezi September Umoja Mataifa umesema kuwa huduma muhimu katika vituo vya afya 300 zimesitishwa na zaidi ya thuluthi tatu ya huduma zao za misaada ya kiutu zimepunguzwa au kuondolewa kabisa.

Soma zaidi:Mamia warejea nyumbani katika ubadilishaji wafungwa Yemen

Saudi Arabia na wafadhili mbali mbali kutoka mataifa ya Kiarabu, wameshindwa kutimiza ahadi zao za msaada wa kiutu wakati ambapo wanakabiliwa na chanagamoto za kiuchumi kutokana na janga la Corona.

Huku hayo yakijiri waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif ameutaka Umoja Mataifa  kuchukua hatua dhidi ya msimamo wa Marekani juu ya vita vilivyotokea tangu 2001.

AFP/AP