1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya 50 wapoteza maisha katika kimbunga

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3fz

NASHVILLE:

Zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha yao na wengi wamejeruhiwa katika kimbunga kikali kilichovuma kusini mwa Marekani.Ripoti za vyombo vya habari zinasema,hicho ni kimbunga kikali kabisa kutokea Marekani tangu kama mwongo mmoja uliopita.

Kimbunga hicho kimepiga katika majimbo ya Tennesse,Arkansas,Kentucky,Alabama na Mississippi lakini Tennesse ni jimbo lililoathirika vibaya zaidi.