1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky atembelea maeneo ya mapigano makali Ukraine

20 Aprili 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametembelea kituo cha kijeshi cha kuongoza mapambano karibu na mji unaokabiliwa na vita wa Chasiv Yar, wakati akielekea kwenye mji wa Donetsk ambao kwa sasa unashuhudia mapigano makali.

https://p.dw.com/p/4f015
Ukraine | Rais wa Ukraine akiwa na maafisa wengine wa serikali kukagua maendelea katia uwanja wa vita.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na baadhi wa maafisa wa serikali wakitembelea maeneo ya mapiganoPicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/AFP

Mji huo wa Chasiv Yar ambao ni jirani na eneo la kimkakati la Bakhmut, ambalo liliwekwa chini ya udhibiti na vikosi vya Urusi takriban mwaka mmoja uliopita baada ya mapigano makali unatazamwa kama shabaha inayofuata kwa Urusi.

Katika siku za hivi karibuni raia Zelensky  amekuwa akitembelea na kufanya ukaguzi katika safu za ulinzi, ambapo alifanya ziara eneo la Dnipro akikaguaa hatua za ulinzi wa miundombinu muhimu ya jiji.

Kupitia katika mtandao wa Telegramu amesema kwamba wanafanya mazungumzo na washirika wa Ukraine ili kupatikana kwa mifumo ya ulinzi wa anga.

Soma pia:

Hivi karibuni vikosi vya Urusi vimeongeza mashambulizi ya anga katika mji wa Dnipro, huku askari wake wakikabiliwa na uhaba wa silaha.