1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani nchini Marekani.

Bergnmann,Christina DW Washington15 Aprili 2008

Kanisa linakabiliwa na changamoto kuhusu uadilifu miongoni mwa waumini wake nchini humo.

https://p.dw.com/p/DiUF
Papa Benedikti XVIPicha: AP

"Mungu ndiye tunayemuamini ,Imani yetu iko kwa Mwenyezi Mungu."Ni maneno yanayokutikana katika sarafu ya Marekani. Imani ya Wamarekani mbele ya Mwenyezi Mungu ndiyo inayowafanya wengi kwenda makanisani mnamo siku ya jumapili akiwemo pia rais wa nchi hiyo. Wamarekani milioni 70 ni waumini wa kanisa Katoliki na ni robo ya wakaazi wa taifa hilo na 38 asili mia huenda kanisani kila jumapili. 41 asili mia hufika kanisa alau mara moja kwa wiki. Papa Benedikt anaipongeza hali hii kama anavyosisitiza David Schindler ,mmoja kati ya viongozi wa kituo cha utamaduni mjini Washington kilichopewa jina la Papa Johanna Paulo II, kuhusu imani ya Wamarekani."Wamarekani wanaposema wanaamini Mungu- Wana amni Mungu. Kuna ukweli halisi katika hilo na nafikiri Papa Benedikti anapendezwa zaidi kujionea hali hii."

Kwa hivyo imani Marekani kawa kasina katoliki ni kubwa, licha ya kwamba lina ukosefu wa utulivu ndani ya kanisa hilo katika Amerika kusini, nchi kama Brazil na Mexico nchi ya tatu yenye waumini wengi wa kikatoliki duniani.

Kwa upande mwengine kanisa Katoliki linakosoa ule mtindo wa waumini wake wa Marekani katika kile linachokiona kuwa ni "mwenendo wa maisha ya kimarekani", maisha ya matumizi bila kipimo na kadhalika. Kwa mujibu wa kituo cha utamaduni cha Pew, 51 asili mia ya wakatoliki wa Marekani kwa mafno wanaunga mkono kuhalalishwa utoaji mimba na 55 asili mia kuunga mkono utafiti juu ya upandikizaji mbegu za uzazi , 42 asili mia ndoa za watu wa jinsia moja na 60 asili mia wanaunga mkono adhabu ya kifo. Kuhusu masuala hayo Bw Schindler anasema,"Inavutia sana , kuona wakati Papa alipozungumzia anakuja Marekani alisema yuko karibu na Wamarekani na Wamarekani wako karibu na moyo wake.Na pia alisema anavutiwa hjinsi wanavyowashughulikia wakongwe na wasio na watu. Kwa hivyo anafikiri atalizungumzia hilo na kukosoa panapopaswa kukosolewa, zaidi msiamamo wa waevangelisti na sio wakatoliki."

Pamoja na yote hayo lakini, kanisa Katoliki linatoa mchango mkubwa katika jamii ya Marekani, kama anavyofafanua mwandishi habari wa masuala ya vatikani John Allen,"Kama taasisi, kanisa Katoliki lina mfumo mkubwa wa elimu binafsi nchini Marekani. Mwaka jana kulikua na watoto milioni 2 na laki 3 walioelimishwa katika shule za kikatoliki nchini Marekani. Kulikua na zaidi ya dola 100 milioni zilizotolewa kama msaada na Kanisa kwa watu masikini. halii hii katika jamii ya Marekani haiwezi kutatuliwa, ikiwa kanisa katoliki nchini humu litashindwa kutoa msaada zaidi."

Katika matatizo yanayolikabili kanisa lenyewe nchini Marekani, Papa Benedikti wa XVI ameelezea kufedheheshwa kwake mno na kashfa za ngono zinazofanywa na mapadiri nchini Marekani na kula kiapo kuwaondoa wanaofanya madhambi hayo katika utumishi wao.

Ziara hii ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa kanisa Katoliki duniani nchini Marekani tangu lilipoanza wimbi la kashfa za kujamiiyana mwaka 2002, na ubakaji, na ambazo zilisababisha kufunguliwa mashitaka yaliomalizika kwa kanisa kulipa zaidi ya dola bilioni 2 kama fidia kwa waliodhurika. Kiongozi huyo alisema kaniasa litafanaya kila liwezeakano kuwachunguza vilivyo wanaomba upadiri, ili wapatikane watu waliowaadilifu na wacha Mungu wa kweli.

Wakati wa ziara hiyo Papa Benedikti pia ataadhimisha mwaka wa 81 wa kuzaliwa na watatu tangu alipochaguliwa kuliongoza kanisa hilo. Mnamo siku ya Ijumaa atauhutubia umoja wa mataifa mataifa akitazamiwa kusisitiza juu ya haja ya amani na haki kote duniani.