1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Rais Ahmadinejad Falme za nchi za kiarabu.

Omar Mutasa11 Mei 2007

Rais MAHMOUD AHMADINEJAD wa Iran anatarajiwa kuwasili hapo kesho Umoja wa falme wa nchi za kiarabu) kwa ziara ya siku mbili, katika nchi hii yenye uhusiano mzuri na Marekani.

https://p.dw.com/p/CB49
Rais Ahmadinejad wa Iran
Rais Ahmadinejad wa IranPicha: AP

Hii ni ziara ya kwanza kiongozi wa Iran kuizuru nchi ya Falme za kiarabu tangu mapinduzi ya kiislamu yafanyike nchini Iran mwaka 1979.

Rais AHMADINEJAD atakutana na Rais wa Falme za kiarabu Sheikh Khalifa bin zayed Al-nahyan baada ya ziara ya hivi karibuni ya waziri wa ulinzi wa Marekani Dick Chenney alieifanya nchini Iraq .

Uhusiano wa serekali ya Abu dhabi na washington kwa jumla haujaharibu uhusiano wa Tehran na Abu dhabi .

Kuna mzozo wa siku nyingi Iran kuvikalia visiwa vya Falme hizo tangu vilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1971.

Visiwa hivo ni Tunb Kubra na Tunb sughra pamoja na kisiwa cha Abu Musa maji ya visiwa hivyo yakielekea katika mlango wa Hurmuz zinapopita meli nyingi katika ghuba .

Saudi Arabia pamoja na wanachama wengine wa Baraza la ushirikiano wa mataifa ya ghuba (AGCC ) wamekua wakiyiuunga mkono Falme hizo mwanchama mwenzao ili yafanyike mazungumzo ya moja kwa moja na Iran kuhusu visiwa hivyo au suala hilo lipelekwe katika mahakama ya kimataifa .

Iran kwa upande wake inasema visiwa hivyo ni milki yake, na wala hapaitaji mjadala wowote kuvizungumzia.

Licha ya mzozo huo, kuna wa Iran wanaoishi Falme za kiarabu zaidi ya Mia 4 elfu huku nchi hizo zikiwa na fungamano kubwa za kibiashara .

.Kufikia May 2006 ambao ndio mwaka wa kiiran, Iran iliagizia kutoka Falme za kiarabu bidhaa za Dollar Billioni 7.67.

Mwaka jana waku wa Iran walimteua aliekua msemaji wa serakali ya Iran, Hamid Reza Asefi kua Balozi wa Iran katika Umoja wa ufalme wa nchi za kiarabu.

Hivi karibuni Iran iliwaonya waku wa Abu dhabi kwa kuwaruhusu wamarekani kuanzisha ubalozi mdogo mjini Dubai ,waku wa Iran walichokiita Marekani kuanzisha mawasiliano na wairan walioko nje ya Iran licha ya Tehran na Washington kutokua na uhusiano wa kibalozi:

Onyo hilo halikuwafurahisha viongozi wa Abu dhabi kwa sababu Iran ililitangaza wazi. Hata hivo viongozi wa Ufalme wa milki za kiarabu wilijaribu kuyapooza malalamiko hayo kwa kuwaachia huru wavuvi kumi na wawili (12 ) wa Iran waliokamatwa kwenye ufuo wa kisiwa cha Abu Musa mapema mwezi huu, huku Rais wa falme za nchi za kiarabu akisema kamwe hawatoruhusu nchi yao kutumiwa kwa malengo mabaya dhidi ya Iran.

Suala la Iran kujenga mtambo wa ki nuclear kusini mwa Iran pia unawapa wasiwasi viongozi wa ghuba, wakihofia uharibifu wa mazingira katika eneo la ghuba, ingawa viongozi wa ghuba nao wamo katika mipango ya kuanzisha mradi wa pamoja wa kinuclear.