1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma kushtakiwa kwa rushwa

29 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Chgl

JOHANNESBURG

Waendesha masataka nchini Afrika Kusini hapo jana wameamuru kiongozi wa chama tawala nchini humo Jacob Zuma ashtakiwe kwa rushwa hapo mwezi wa Augusti mwakani hatua ambayo itaathiri harakati zake za kuwania urais wa nchi hiyo.

Zuma alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ANC wiki iliopita.Kumshtaki huko kunaweza kuzidisha mgawanyiko ndani ya chama hicho tawala na kuvuruga matumaini yake ya kuchukuwa nafasi ya Rais Thabo mbeki ambaye lazima an’gatuke hapo mwaka 2009.

Wakili wa utetezi Michael Hulley ambaye ameishutumu Mamlaka ya Taifa ya Kuendesha Mashtaka na kitengo maalum cha Upelelezi cha Scorpio kwa kujaribu kumharibia jina Zuma amesema Zuma anashtakiwa kwa magendo,kuhalalisha matumizi ya fedha zilizopatikana kwa njia ya haramu,udanganyifu na rushwa.

Kesi hiyo ya Zuma itaanza kusikilizwa hapo tarehe 14 mwezi wa Augusti mwaka 2008.