1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Kikosi cha Afrika chaongeza muda Dafur

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpL

Umoja wa Afrika umeongeza muda wa mamlaka ya kikosi chake cha kulinda amani huko Dafur nchini Sudan hadi mwishoni mwa mwaka huu na kusema kwamba inatumai juhudi za kuweka kikosi mchanganyiko cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika jimbo la Dafur zitaharakishwa.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika pia limetowa wito wa msaada wa kifedha na vifaa kwa operesheni za kikosi chake hicho katika jimbo la Dafur ambapo wakati fulani hakikulipwa mshahara kwa miezi mitatu.

Kufuatia juhudi nzito za kidiplomasia za miezi kadhaa Sudan ilikubali wiki iliopita kuwekwa kwa kikosi mchanganyiko cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 23,000 pamoja na polisi kuimarisha kikosi cha wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika walioko Dafur.