1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:AU walaani shambulio dhidi ya askari wake nchini Sudan

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKm

Umoja wa Afrika umetoa wito wa kupelekwa mwezi huu nchini Sudan kwa kikosi cha kwanza cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, kufuatia shambulizi la kikaktili dhidi ya kikosi cha Umoja wa Afrika ambapo wanajeshi kumi waliuawa.

Mkuu wa Baraza la Usalama na Amani la Umoja huo lenye wanachama 15, Said Djinnit amesema kuwa Umoja wa Afrika unategemea kuwa awamu ya kwanza ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa itawasili nchini Sudan mwezi huu.

Kwa upande wake Balozi wa Malawi ambayo ni mwenyekiti wa baraza hilo, James Kalilangwe alitoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa maafisa wa kijeshi wa nchi zilizochangia askari kwenye kikosi hicho ili kutathmini uwezo wa kikosi hicho.

Pia amesema kuwa Umoja wa Afrika ni lazima umepitie upya wajibu wake nchini Sudan ambao kwa sasa ni kutumia nguvu kwa nia ya kujilinda.