1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Uturuki yatafakari hatua ya kijeshi kwa Iraq

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Db

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amekuwa na mazungunzo ya dharura kutafakari shambulio la kijeshi dhidi ya makambi ya waasi wa Kikurdi ndani ya Iraq kutokana na shambulio la wapiganaji hao wa chini kwa chini walilofanya kwa wanajeshi wa Uturuki.

Baada ya mazungumzo hayo serikali ya Uturuki imesema iko tayari kulipa gharama yoyote ile kuilinda nchi hiyo.

Akizungumzia mgogoro huo Waziri Mkuu wa Uturuki Erdogan amesem ni jambo lisilokubalika kwa rais wa nchi Jalal Talabani kuvumilia ugaidi na nchi yake Uturuki haiwezi kujadiliana na nchi ambayo hailitambuwi kundi la PKK kuwa ni kundi la magaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ameitaka Uturuki kuwa na uvumilivu kwa kutochukuwa hatua ya kijeshi.Kwa upande wake serikali ya Ujerumani imeelani shambulio la kundi la PKK lililouwa wanajeshi 17 wa Uturuki na kujeruhi wengine 16.

Maafisa wa kijeshi wa Uturuki wamesema vikosi vyao vimejibu mapigo shambulio hilo la waasi wa Kikurdi na kuwauwa 32 na pia kushambulia kwa mizinga kwenye maeneo ya mpakani mwa Iraq.

Uturuki imekuwa ikitishia kuvamia kaskazini mwa Iraq kuchukuwa hatua dhidi ya waasi wa Kikurdi wanaokadiriwa kufikia 3,500.