1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO:Uchaguzi wa rais wafanyika nchini Mali

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5u

Watua wa Mali wanapiga kura kumchagua rais ambapo wajumbe wanane wamesimama katika uchaguzi.

Rais wa sasa Amadou Toumani anaewania kipindi cha pili cha urais anasemakana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda katika uchaguzi huo.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa idadi ya wapiga kura inatarajiwa kuwa ndogo, kwa sababu wastahiki wengi hawajaenda kuchukua kadi za kujiandikisha.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanatumai kwamba uchaguzi huo utaimarisha demokrasia nchini Mali.