1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yafanya mazungumzo na mshambuliaji Randal Kolo Muani

2 Mei 2023

Bayern Munich wamefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Randal Kolo Muani juu ya uwezekano wa kujiunga na mabingwa hao watetezi wa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/4QnVu
Champions League Sporting Lissabon vs Eintracht Frankfurt
Picha: Carlos Costa/AFP/Getty Images

Ripoti ya shirika la Habari la Sky imeeleza kuwa, mazungumzo hayo yalikuwa mazuri japo hadi sasa hakuna maelewano yoyote yaliyoafikiwa.

Vilabu kadhaa vya Ulaya pia vinammezea mate mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa aliyefunga mabao 13 ndani ya Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.

"Bila shaka Randal amezivutia timu nyingi kutokana na umahiri wake uwanjani. Lakini hadi sasa hatujapokea ombi lolote la usajili, sio kutoka kwa Bayern Munich au klabu nyingine,” Mkurugenzi wa michezo wa Frankfurt MarkusKrösche aliiambia televisheni ya Sky hivi majuzi.

Kolo Muani alijiunga na Frankfurt akitokea Nantes huku akiwa na mkataba wa kuichezea mabingwa hao wa Ligi ya Ulaya hadi mwaka 2027.

Bayern Munich pia iko sokoni kuwawinda washambuliaji Harry Kane wa Tottenham Hotspurs na Victor Osimhen wa Napoli ili kujaza nafasi ya Robert Lewandowski aliyejiunga na Barcelona msimu uliopita.