1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki mpya yazinduliwa Amerika ya Kusini

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZWB

Rais Hugo Chavez wa Venezuela na viongozi wengine 6 wa nchi za Amerika ya Kusini wamezindua benki ya maendeleo ya kanda hiyo,ili kupunguza kutegemea benki za Marekani.Benki hiyo ikiitwa Benki ya Kusini,inaanzishwa kwa mtaji wa Dola bilioni 7 na itatoa mikopo kwa nchi za kanda hiyo bila ya masharti magumu kinyume na Benki Kuu ya Dunia,Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF au Benki ya Maendeleo ya Marekani.

Hati ya kuanzisha benki hiyo mpya imetiwa saini na marais wa Argentina,Bolivia,Brazil,Ecuador, Paraguay na Venezuela na pia mjumbe wa Uruguay. Rais wa Brazil,Luiz Inacio Lula da Silva amesema,kuzinduliwa kwa benki hiyo ni hatua inayoimarisha umoja wa nchi za kanda ya kusini.