1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Serikali ya Schroeder yapata pigo jipya la kashfa ya viza

6 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZ6

Serikali ya Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani imepata pigo jipya leo hii kutokana na repoti kwamba Waziri wa mambo ya nje Yoshcka Fischer alikuwa akijuwa na mapema kwamba kulikuwepo na ukiukaji wa taratibu za visa miaka mitatu kabla ya kuchukuwa hatua za kuusitisha.

Wakati uchunguzi wa maoni ukionyesha kushuka kwa umashuhuri wa serikali hiyo kutokana na kashfa hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa jimbo muhimu hapo mwezi wa Mei gazeti la Jumapili la Frankfurter Allgemeine limesema Fischer alikuwa akijuwa hapo mwaka 2000 kwamba wahalifu wa Ukraine walikuwa ni miongoni mwa hao wanaopatiwa visa za kuingia Ujerumani.

Kashfa hiyo ambayo kwayo Fischer amekubali kubeba lawama na kukiri kwamba wakati fulani alifikiria kujiuzulu ni suala gumu ambalo limesababisha mvutano kati ya chama chake cha Kijani na kile cha Schroeder cha SPD na pia linakuja katika wakati mbaya ambapo Rais mpya wa Ukraine Viktor Yuschenko anaitembelea Ujerumani wiki hii na atazungumza na bunge hapo Jumaatano