1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Merkel kuanza ziara ya Afrika

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKn

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kesho anaanza ziara ya siku tano barani afrika itakayomchukua katika nchi za Liberia, Ethiopea na Afrika Kusini.

Bi Merkel anatarajiwa kuzungumzia juu ya masuala ya haki za binaadamu pamoja na hali nchini Zimbabwe.

Pia atatumia ziara hiyo kuimarisha zaidi uhusiano kati ya afrika na Ujerumani..