1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden asema kuisaidia Ukraine ni jukumu la ulimwengu mzima

Lilian Mtono
26 Januari 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amewashukuru washirika wa magharibi kwa kuisaidia kijeshi Ukraine, wakati akitangaza kwamba Marekani nayo itapeleka vifaru 31 aina ya Abrams nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Mic4
Präsident Joe Biden zu Ukraine-Hilfe
Picha: Susan Walsh/AP/picture alliance

Biden amesema kuisaidia Ukraine kupambana na uvamizi wa Urusi na kulinda uhuru wake ni jukumu la ulimwengu mzima.

''Tangazo la leo linatokana na kazi kubwa na jukumu la mataifa kote ulimwenguni, yakiongozwa na Marekani kuisaidia Ukraine kulinda uhuru wa nchi yake. Na hii ndio maana yake.. kuisaidia Ukraine kutetea na kuilinda ardhi yake. Sio kitisho cha kuishambulia Urusi. Hakuna kitisho cha kuishambulia Urusi. Ikiwa wanajeshi wa Urusi watarudi kwao, basi watakuwa mahali wanakostahili. Na hivi vita vingekuwa vimekwisha.'' alisema Biden.

Kulingana na maafisa wa ngazi ya juu, Marekani itapeleka vifaru 31 chapa Abrams M1, hatua iliyohitimisha mabishano ya miezi kadhaa ndani ya serikali ya Biden kwamba ni vigumu kwa wanajeshi wa Ukraine kuvitumia na kuvitunza vifaru hivyo.