1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo na vita visivyokwisha dhidi ya Ebola

Saleh Mwanamilongo
4 Juni 2020

Congo inakabiliwa na ugonjwa mpya wa Ebola huko kaskazini magharibi mwa nchi. Ni kwa mara ya saba sasa tangu mwaka 2007 Congo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, lakini taifa hilo imejiandaa vyema mara hii ili kukabiliana nao.

https://p.dw.com/p/3dGw5
Mtoa huduma wa afya wa shirika la afya ulimwenguni WHO akitoa chanjo mjini Mbandaka,jimboni Equateur,magharibi mwa Congo.
Mtoa huduma wa afya wa shirika la afya ulimwenguni WHO akitoa chanjo mjini Mbandaka,jimboni Equateur,magharibi mwa Congo.Picha: picture-alliance/AP/S. Mednick

Ugonjwa wa Ebola ambao kwa miaka miwili sasa unaendelea huko mashariki mwa Congo umedhibitiwa kabla ya kuripotiwa kwa visa vipya mbali na eneo hilo, huko kaskazini magharibi mwa nchi. Maeneo hayo mawili yana umbali wa kilomita 1200.

Wizara ya afya ya Congo ilitangaza Jumatatu kwamba watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa huo. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto, UNICEF, ni kwamba watu 5 walikufa na wengine wa nne kuambukizwa.

Waziri wa afya Eteni Longondo aliiambia DW kwamba watu 12 wamedhaniwa kuambukizwa na ugonjwa huo hadi Jumanne mjini Mbandaka, jimboni Equateur.

Siyo mara ya kwanza jimbo hilo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, miaka miwili iliyopita ugonjwa wa Ebola uliodumu miezi miwili na nusu ulizuka na kuambukiza watu 54 na kusababisha vifo 33.

''Ni alama nzuri kuona kwamba ugonjwa umefahamika. Watu wanaofanya kazi kwenye eneo hilo wamefahamu vyema dalili za ugonjwa wa Ebola,'' alisema Natalie Roberts wa shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka. Roberts anaamini kwamba ugonjwa huo utadhibitiwa haraka iwezekanavyo.

Congo ya fanya vyema katika kupambana na Ebola

Kwa mujibu wa shirika la UNICEF watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni baina ya Mei 18 hadi Mei 30.

Kongo Mbandaka Impfung gegen Ebola
Picha: Getty Images/AFP/J.D. Kannah

Hatua kubwa imepigwa katika juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola kufuatia kuweko na chanjo. Mwishoni mwa mwaka 2019, Marekani na Umoja wa Ulaya zilithibitisha chanjo ya Ervebo. Kwa mujibu wa kampuni ya Merck, Congo, Ghana Zambia na Burundi ziliruhusu matumizi ya chanjo hiyo. Wizara ya Congo ya Afya inasema kwamba chanjo hiyo itapelekwa pia huko jimboni Equaeur. Chanjo hiyo ilitumiwa huko huko Equateur miaka miwili iliopita, zaidi ya watu elfu moja wakiwemo watoa huduma walipewa chanjo hiyo.

Profesa Marylyn Addo, mtafiti mkuu kwenye chuo kikuu cha kiganga cha Hamburg-Eppendorf, kilichoendesha moja wapo ya utafiti kuhusu ufanisi wa chanjo hiyo amesema kwamba wale waliopewa chanjo hiyo mwaka 2018 wanaweza kuwa na kinga dhidi ya ugonjwa huo hivi sasa. Aidha, hakuna data inayoonyesha muda gani chanjo hiyo inaweza kumkinga mtu aliyepewa.

Hadi sasa, chanjo hiyo imetolewa kwa ajili ya kinga dhidi ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola. Unawapa chanjo watu wote waliokuwa na mawasiliano na wagonjwa wa Ebola na majirani zao, inasaidia kudhibiti ugonjwa, alisema Addo.

Lakini licha ya vita dhidi ya ugonjwa huo Ebola itajitokeza kila mara, kwa sababu virusi vinapatikana ndani ya wanyama, aliendelea kusema profesa Addo.

Congo imejitahidi kupambana na ugonjwa wa ebola mara kadhaa ulipozuka hata bila kuweko na chanjo. Lakini vita dhidi ya magonjwa mengine havitakiwi kusahaulika. Mwaka 2019 zaidi ya watu elfu sita nchini Congo walifariki kutokana na surua, idadi kubwa kuliko Ebola.