1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Denmark yasitisha msaada kwa Tanzania

Sekione Kitojo
15 Novemba 2018

Denmark  kuzuia sehemu kubwa ya fedha za misaada inayotoa kwa  Tanzania kutokana na wasiwasi wa ukiukaji wa haki za binadamu na  matamshi ya chuki dhidi ya binadamu wengine yaliyotolewa na afisa wa serikali.

https://p.dw.com/p/38Hat
Tansania Daressalam Paul Makonda
Picha: DW/S. Khamis

Denmark  ambayo  ni nchi  ya  pili kwa  ufadhili kwa Tanzania  itazuwia  sehemu  kubwa ya  fedha  za  misaada inayotoa  kwa  nchi  hiyo  kutokana  na  wasiwasi  wa ukiukaji  wa  haki  za  binadamu pamoja  na  matamshi ambayo  hayakubaliki  ya  chuki  dhidi  ya  binadamu wengine yaliyotolewa  na afisa  wa  serikali.

Hayo  yameelezwa  na  waziri  wa  misaada  ya  maendeleo wa  Denmark  bungeni  jana. Waziri  wa  ushirikiano  wa maendeleo  Ulla Tornaes  ameeleza  kwamba  ana  wasi wasi  mkubwa  kuhusu hali hasi  inayojitokeza  nchini Tanzania, hususan  matamshi  ya  chuki  dhidi  ya  wapenzi wa jinsia moja,  yaliyotolewa  na  mkuu  wa  mkoa.

Shirika  la habari  la  Reuters  lilisema  kuwa  halikuweza kuzungumza  na maafisa  wa  serikali  ya  Tanzania ili kutoa  maelezo  yao kuhusu  suala  hilo.