1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUturuki

Erdogan: Wanachama 1,000 wa Hamas wanapokea matibabu Uturuki

14 Mei 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema zaidi ya wanachama 1,000 wa kundi la Hamas wanapokea matibabu nchini Uturuki.

https://p.dw.com/p/4fokI
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Umit Bektas/REUTERS

Rais Erdogan ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.

Kiongozi huyo wa Uturuki hata hivyo hakutoa maelezo zaidi juu ya sehemu walikojeruhiwa wanachama hao wa Hamas au jinsi walivyofika Uturuki.

Soma pia:  Hamas yakubali kusitisha mapigano, Israel yaishambulia Rafah

Erdogan amewahi kuieleza Hamas kama kundi la ukombozi linalotetea haki za Wapalestina.

Hata hivo, Marekani, Uingereza, Israel na mataifa mengine yenye nguvu yameliorodesha Hamas kama kundi la kigaidi.