1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yatoa onyo juu ya uchunguzi wa vita vya Kaskazini

Bruce Amani
15 Februari 2023

Ethiopia imeonya kuwa juhudi za wachunguzi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuchunguza unyanyasaji uliofanywa wakati wa vita vya kaskazini mwa nchi hiyo, huenda zikahujumu hatua zilizopigwa za makubaliano ya amani

https://p.dw.com/p/4NX7J
Äthiopien | Demeke Mekonnen Hassen
Picha: Graham Carlow/Creative Commons

Katika ripoti yake ya kwanza iliyochapishwa Septemba mwaka jana, Tume ya Watalaamu wa Haki za Binaadamu kuhusu Ethiopia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilisema ilikuta ushahidi wa ukiukaji kutoka pande zote ambao unaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu. 

Waasi wa Tigray waanza kuzisalimisha silaha zao nzito

Serikali ya Ethiopia iliipinga ripoti hiyo na imeanzisha juhudi za kidiplomasia ili kupata uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa katika jaribio lake la kuizuia tume hiyo kuendelea na kazi yake.

Jeshi la kikanda lajiondoa mji wa kimkati wa Shire-Tigray

Naibu waziri mkuu wa Ethiopia na Waziri wa Mambo ya Kigeni Demeke Mekonnen amesema tume hiyo huenda ikahujumu mchakato wa amani ulioongozwa na Umoja wa Afrika na utekelezwaji wa Makubaliano ya Amani ya Pretoria kwa kutumia maneno ya uchochezi.