1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yamfungia mwamuzi wa Tanzania

Sekione Kitojo Mhariri: Yusuf Saumu
27 Februari 2019

Mwamuzi kwa jina Oden Charles Mbaga kutoka Tanzania amepigwa marufuku ya maisha na shirikisho la kandanda duniani FIFA kwa kupokea  hongo.

https://p.dw.com/p/3EBZP
Symbolbild FIFA
Picha: picture-alliance/dpa/KEYSTONE/E. Leanza

Shirikisho  la  kandanda  duniani  FIFA  limesema  kamati yake  ya  maadili  imeweka marufuku  ya  maisha  dhidi  ya mwamuzi  Oden Charles Mbaga  kutoka  Tanzania  kwa kupokea  hongo. Shirikisho  la  FIFA  limesema  Mbaga pia amepigwa  faini  ya  dola  laki  mbili.

Haijafahamika  wazi  ni  vipi  FIFA  inaweza  kutekeleza faini  hiyo  kwa  ajili  ya  tabia  ambayo  ni  kinyume  na maadili. Bila  ya  kutoa  maelezo  ya  rushwa, FIFA imesema  Mbaga  alikiuka  sheria  ya  mwaka  2009  ya maadili  licha  ya  kuwa  uchunguzi  ulianzishwa  mwezi Julai mwaka  jana.

Mbaga  anaripotiwa  kuhusika  na  mtu  anayetuhumiwa kupanga  matokeo  Wilson Perumal  wa  Singapore, ambaye  amehusika  katika  kuwapata  waamuzi katika michezo  ya  kirafiki  katika  utabiri  wa  matokeo  bandia.