1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ishara njema katika suala la kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Palastina

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBK

Gaza/Jerusalem

Wawakilishi wa Israel na wale wa Hamas wamethiibitisha ripoti kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika juhudi za kuachiliwa huru mwanajeshi wa kiisrael Gilad Schalit anaeshikiliwa mateka tangu miezi tisaa iliyopita.Msemaji wa Hamas FAWZI BARHUM amesema kuna dalili za kutia moyo katika mazungumzo ya kubadilishana wafungwa.Kupitia upatanishi wa Misri,Israel imekabidhiwa orodha ya majina ya wafungwa wa kipalastina wanaobidi kuachiliwa huru.Israel inasubiriwa kutoa jibu.Kwa mujibu wa duru za wapalastina,Hamas wanadai wapalastina zaidi ya elfu moja waachiwe huru.Muakilishi wa ngazi ya juu wa serikali ya Israel amethibitisha pia kupitia Radio Israel,”kuna ishara za maendeleo”,amesisitiza hata hivyo “bado kuna mengi ya kufanya kabla ya kuafikiana kubadilishana wafungwa.”