1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yaendeleza mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza

Tatu Karema
11 Oktoba 2023

Israel imeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza kwa siku ya tano mfululizo baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu kutangaza vita dhidi ya vuguvugu la Hamas linalotawala ukanda huo

https://p.dw.com/p/4XNUp
Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel katika  mji wa Gaza Jumanne, Oktoba 10, 2023.
Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Gaza Picha: Hassan Eslaiah/AP/picture alliance

Mashambulizi hayo ya Israel yanafuatia mashambulizi makubwa yaliofanywa na vuguvugu la Hamas ndani ya Israel mwishoni mwa juma, huku mashirika ya kiutu yakitafuta njia za kuwasaidia raia waliokwama katika vita hivyo.

Soma pia:Upinzani nchini Israel waungana kukabiliana na Hamas

Makabiliano ya risasi kati ya vikosi vya Israel na wanamgambo wa Palestina yamesababisha vifo vya wanamgambo watatu katika mji wa Ashkelon kusini mwa Israel.

Jeshi la Israel linaendelea kuwatafuta wapiganaji wa kundi la Hamas

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihudhuria mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri katika ofisi yake mjini Jerusalem, Septemba 27, 2023
Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan/Pool via REUTERS

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wakisaidiwa na helikopta na ndege zinaondeshwa bila rubani wamefyetuliana risasi na magaidi kadhaa katika eneo la viwanda la Ashkelon, kilomita kadhaa Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku wakiendelea kuwatafuta wapiganaji wa kundi la Hamas waliojificha.

Soma pia:Israel yakomboa maeneo ya mpaka na Gaza

Ndege ya kwanza ya silaha za Marekani yatua Israel

Jeshi la Israel pia limesema kuwa ndege ya kwanza iliyobeba silaha za Marekani imetua nchini humo baada ya Marekani kusema itatuma mahitaji mapya ya ulinzi wa anga, risasi na msaada mwingine wa kiusalama kwa mshirika wake dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina kwa kundi la Hamas.