1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Chama tawala chashinda uchaguzi Uturuki

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg2

Wafuasi wa chama kinachotawala nchini Uturuki cha AKP wamekuwa wakishangilia baada ya matokeo yasiyo rasmi ya kwamba chama hicho kimeshinda katika uchaguzi mkuu wa jana.

Taarifa zinasema kuwa chama hicho cha kiislam cha AKP kimepata asilimia 47 ya kura zote, huku chama kikuu cha upinzani cha RPP kikipata asilimia 21.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungmzia juu ya ushindi wa chama chake alisema kuwa ni ushindi kwa demokrasia nchini humo.

Upinzani umesema kuwa ushindi wa chama hicho cha AKP unahatarisha utaratibu wa uturuki kutoegemea upande wa kidini.

Katika uchaguzi huo wagombea binafsi 27 wakiwemo wa kutoka kabila la kikurd 24 walifanikiwa kushinda viti vya ubunge.