1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jenerali Nguema aapishwa kuwa rais wa mpito wa Gabon

Sudi Mnette
4 Septemba 2023

Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye aliongoza mapinduzi wiki iliyopita yaliouondoa utawala wa kiukoo wa Gabon uliodumu kwa miaka 56, amekula kipao chake cha kuwa rais wa mpito kwa kutoa ahadi nyingi.

https://p.dw.com/p/4VwoO
Gabun, Libreville | General Brice Oligui Nguema wird als Interimspräsident vereidigt
Picha: AFP/Getty Images

Rais Nguema ameahadi ya kufanikisha uchaguzi huru, wa wazi na wa kuaminika katika kurejesha utawala wa kiraia lakini bila kuanisha muda wa ukomo wa ahadi yake katika kufanikisha jambo hilo hilo.

Nguema ameonesha pia dhamira ya kuwasamehe wafungwa wa kisiasa, katika hotuba ambayo alisisitiza kuwa mapinduzi hayo yameiokoa Gabon kutokana na umwagaji damu ambao ungeweza kutokea baada ya uchaguzi ambao uligubikwa na ulaghai. Bila kutaja tarehe ya uchaguzi huko katika hotuba yake baada ya kuapishwa. Amesema uchaguzi ulioahidiwa ndio utakuwa msingi wa kurejesha madaraka kwa raia.

Makundi ya muhimu kushiriki uundwaji wa katiba mpya.

Gabun, Libreville | General Brice Oligui Nguema wird als Interimspräsident vereidigt
Rais wa Mpito wa Gabon akihutubia taifa baada ya kula kiapo cha kuongoza kwa mpitoPicha: Gerauds Wilfried Obangome/REUTERS

Alisema atayashirikisha makundi yote muhimu ya nchini Gabon kwa lengo la kuanza uandishi wa katiba mpya, ambayo baadae itapitishwa kwa kura ya maoni. Katika hotuba yake alitetea vikali mapinduzi hayo, akisema jeshi lilichukua hatua ya kuokoa maisha kufuatia "mchakato wa uchaguzi ambao bila shaka ulikuwa umejaa." aliongeza kusema "Baada ya kipindi cha mpito, kwa kuungwa mkono na washirika wote wa maendeleo wa Gabon, tunakusudia kukabidhi madaraka kwa raia kwa kuandaa chaguzi mpya, huru, za wazi na za kuaminika katika mazingira ya amani kwa jamii.

Nguema mwenye umri wa miaka 48, aliyekua amevalia vazi jekundu ambalo ni mahususi kwa hafla za kijeshi, pia alisema atatoa muongozo kwa serikali ijayo kufikiria njia za kuwaachilia wafungwa wa kiasiasa na kutoa ridhaa ya kurejea nchini humo baadhi ya raia wa taifa hilo ambao wanaishi uhamishoni.  Akimnukuu shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini Desmond Tutu, alisema: "Ikiwa hauegemei upande wowote katika hali ya dhuluma, umechagua upande wa dhalimu."

Kiongozi huyo wakijeshi alikuwa anaokekana kama akiyaoneshea kidole "mashirika ya kimataifa," ambayo hakuyataja moja kwa moja, kwa kukosoa unyakuzi wake wa madaraka wa kijeshi.

Ali Bongo bado yupo kizuizini.

Baada ya kuzuiliwa rais aliyepinduliwa Ali Bongo katika kizuizi cha nyumbani, viongozi hao wa mapinduzi Jumatano iliyopita walisema wamevunja taasisi zote za kiaifa, kufuta matokeo ya uchaguzi na kufunga mipaka kwa muda. Hadi katika hatua hii ya sasa ya kiapo, nchi baadhi ya hazijamtambua Nguema kama kiongozi halali wa Gabon na wakimpa na shinikizo la kufanikisha mipango yake ya kurejesha haraka utawala wa kiraia.

Soma zaidi;Jenerali Brice Oligui Nguema kuapishwa leo

Gabon inaungana na Mali, Guinea, Sudan, Burkina Faso na Niger katika safu ya nchi za Kiafrika ambazo zimepitia mapinduzi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hali ambayo imekuwa inatoa onyo kwa mataifa mengine ya Afrika.

AFP