1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jenin:Kiongozi wa kundi la Jihad auwawa

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPw

Wanajeshi wa kikosi maalum cha Israel waliovalia kama Wapalestina, wamemuuwa Kiongozi wa bawa la kijeshi la chama cha Kiislamu cha Jihad katika mji wa kasjkazini mwa ukingo wa magharibi wa Jenin.

Mahmud Qassem Abu Obeid aliyekua na umri wa miaka 25 aliuwawa wanajeshi hao wa Israel walipolivamia gari lake wakilishambulia kwa mlolongo wa risasi. Tukio hilo limezuka siku moja baada ya polisi nchini Israel kumtia nguvuni mwanaharakati mmoja wa chama cha Jihad kutoka mji wa Jenin, katika nyumba moja kwenye kitongoji cha mjini Tel Aviv, akishukiwa kuandaa shambulio la kujitoa mhanga.