1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Jeshi la Israel layafunga maeneo ya Wapalestina

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQc

Jeshi la Israel limetangaza limeyafunga maeneo ya Wapalestina kwa muda usiojulikana wakati wa kuanza mwaka mpya wa kiyahudi.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema kwa mujibu wa uamuzi wa waziri wa ulinzi wa Israel na ikizingatiwa tathimini ya hali ya usalama, maeneo ya Judea, Samaria na Ukanda wa Gaza yamefungwa kuanzia saa sita usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo Israel imesema itaruhusu Wapalestina wanaohitaji misaada ya kiutu na huduma za dharura wapite.

Jeshi la Israel limesema Wapalestina takriban 1,600 walio katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan wataruhusiwa kuingia Israel kuvuna zeituni.

Wakati huo huo, Israel imewaonya vikali wanamgambo wa kipalestina katika Ukanda wa Gaza walioishambulia kwa maroketi kambi ya jeshi la Israel ya Zikim na kuwajeruhiwa wanejeshi takriban 69.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni, amesema Israel ina uwezo wa kijeshi kukabiliana na wanamgambo katika Ukanda wa Gaza.